Winga wa Manchester City Raheem Sterling ambaye amejiunga na timu
hiyo baada ya kununuliwa toka Liverpool ameonekana kuanza kuwavutia
mashabiki wa klabu yake mpya baada ya kitendo chake cha kugawa jezi kwa
shabiki mdogo baada ya mchezo wake wa kwanza kwenye ligi kuu ya England .
Sterling ambaye alinunuliwa katika dili la paundi milioni 49 alivua
jezi yake baada ya mchezo dhidi ya Westbromwich Albion na kwenda moja
kwa moja jukwaani ambapo aliikabidhi jezi hiyo kwa shabiki mmoja ambaye
alionekana kufurahia kitendo hicho .
Sterling akiruka uzio kwenda kutoa jezi kwa shabiki wa Man City.
Sterling alifanya kitendo hicho kwenye mchezo ambao Man City
ilishinda kwa matokeo ya 3-0 matokeo ambayo yamewafanya waongoze ligi
katika wiki yake ya kwanza huku mabingwa watetezi wa ligi hiyo Chelsea
wakibanwa mbavu .
Sterling alivua jezi yake na kwenda kuigawa kwa shabiki wa Man City.