USAILI VIDEO YA DIAMOND KUFANYIKA NYUMBANI LOUNGE!!
USAILI wa wanamitindo na wachezaji watakaonekana kwenye video
mpya ya msanii wa Kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’
unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, Kinondoni, Dar es
Salaam.
Akizungumza mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni One
Touch Solutions, Petter Mwendapole amesema wamechagua Nyumbani Lounge kwa kuwa
ni rahisi kufikika na watu wengi kwa urahisi.
“Mchujo wa wale watakaotaka kushiriki kwenye video hiyo mpya ya
Diamond Platnumz itafanyika nyumbani, kuna mambo mengi pia yamechangia katika
kufanya usaili huo Nyumbani.
“Nyumbani lounge inamilikiwa na msanii mwingine wa kimataifa wa
Tanzania Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’, na huyu ni msanii wa kwanza kuweza
kusimama mwenyewe na kujitegemea, mchango wake ni mkubwa katika ulimwengu wa
muziki wa kizazi kipya Tanzania, wanaohitajika kuja kwenye usaili pia
tunatarajia watakuja kujitegemea kwa kuafata nyayo za JD,” alisema.
Mwendapole alisema, uongozi wa Nyumbani Lounge chini ya
Mkurugenzi wake Gadner G Habash ulipopewa wazo la kufanyika usaili huo
hawakusita na walipokea kwa mikono miwili na kuahidi kushirikiana na timu nzima
ya Diamond katika kuhakikisha usaili huo unafanikiwa.
Mkurugenzi huyo pia alisema watu wengi wamekuwa wakiuliza
maswali kuhusu malipo na vigezo ambavyo vitatumika katika kuwapata watu
watakaoshiriki kwenye usaili huo ambapo alieleza kuwa watakaochaguliwa
watalipwa na ndio maana kumewekwa usaili.
“Wote watakaochaguliwa kuonekana kwenye video hiyo watalipwa,
mpango wa Diamond ni kutengeneza ajira kwa watu wengine si kuuza sura kama watu
wengi wanavyowaita wale wanaonekana kwenye video, vigezo pale kutakuwa wabunifu
wa mitindo ambao wamesomea kazi zao, kutakuwa na walimu wa muziki, kutakuwa na
watu ambao wamesomea mambo ya uongozaji wa picha na kurekodi, hii timu
itaangalia vitu vingi kupata washindi,” alisema.
Alisema washiriki wanatakiwa kuja na nguo za kuogelea, kutokea,
ambapo pia kutakuwa na Red Carpet. Hii ni mara ya kwanza kwa watu wanaotakiwa
kuonekana kwenye video kufanyiwa usaili.
HUU NDO UKWELII KUHUSIANA NA DIAMOND NA WEMA SEPETU......!!!!!!!!
akiongea DIAMOND PLATNUM KATIKA KINYWA CHAKE.....Najua watu wengi sana mnapenda Couple hii na furaha yenu ni kutuona wawili sisi tukiwa kwenye Mahusiano ya kimapenzi.... na mmekua mkifurahi sana na story za hapa na pale mkiskia kua wawili sisi tumekua pamoja na hata pindi mkituona tuko pamoja pia Mmekua mkishangilia na kufurahi... bt ukweli ni kwamba Mimi na Wema hivi sasa si Wapenzi tumekua ni kama Dada na Kaka ama marafki tu wa kawaida ambao tunashirikiana katika kazi mbalimbali za sanaa na za n'nje ya sanaa, katika harakati za kujenga Taifa Letu... Pia ni vizuri ningependa mfahamu kwamba Wema ana Mpenzi wake ambae namfaham na tunaheshimiana kama mtu na Shemeji yake........So das' de Truth abt me and Her!... and Get ready! kwa kazi tofautitofauti ambazo soon zitadondoka....
HUU NDO UNYAMA ALIONESHA MWANA MUZIKI SHETTA DARSTAMINA KWA BINTI YAKE KIPENZI.....!!!!!!!!!
Subscribe to:
Posts (Atom)