EXCLUSIVE: HII NDIO KAULI YA MWISHO YA ORIJINO KOMEDI KUHUSU VENGU!





Orijino Komedi wakiwa na Vengu wa mwisho kulia, hapa ilikua kabla hajaanza kuugua.
Nafaham ni watanzania wengi ambao wanalo hili swali kama mimi, toka tulipoacha kumuona msanii/mchekeshaji Vengu kwenye ORIJINO KOMEDI baada ya kuumwa, zilizuka stori nyingi sana lakini stori ya mwisho mimi kuipata ni kwamba alisharudi Tanzania akitokea kwenye matibabu India na afya yake inaendelea vizuri.
Baada ya kufahamu hivyo nikawa na kiu ya kutaka kujua ni lini tutaanza kumuona akichekesha tena ndani ya Orijino Komedi hivyo nikapata nafasi ya kuzungumza na Wakuvanga ambae ndio mkurugenzi wa kampuni inayoisimamia Orijino Komedi.
Namkariri akisema “ukweli niwe muwazi, kwa afya yake na tatizo alilonalo tunazungumzia tatizo la mshipa wa fahamu, tunazungumzia kitu kinaitwa ubongo, hayo matatizo yanachukua muda mrefu sana ukizungumza ukiwaambia watanzania kwamba atarudi hivi karibuni unakua unajidanganya wewe na watanzania wenzio, ndio maana siku zote tunasema ukiwa na nafasi ya kumuombea mtu unaempenda muombee, mi siwezi kuahidi kwamba labda atarudi mwezi ujao au mwaka ujao”
Kuhusu kutafuta mtu wa kuziba nafasi ya Vengu, Wakuvanga amesema “tutaendelea kuwa na jina la Vengu maisha yote ya Komedi, kwetu sisi iko tofauti kidogo sisi tumeapa.. ndivyo tunavyoishi, tuko saba mpaka tunakufa.. kuongezeka kwa mtu labda sisi tukae pembeni tuwatafute watu wengine lakini tutaendelea kuwa saba, hata maeneo tunayoishi na jinsi tunavyoishi mara nyingi tunaishi tuko saba, akipungua mmoja bado tuko saba”

BAGHDAD AVUKA BODA.


Msanii aliezuiliwa kufanya show, kupiga intaview, wala kolabo ili kupisha muda wa kuanda ngoma ambazo yuko mbioni kuingia both beat produced by c.e.o wa chofacho rec studio iliyoko marekani ambae ndio inamsimamia msanii huyo kwa sasa imeamua kufungua website kwa ajili ya kuweka mambo yanayohusu mziki, maisha na harkati anazozifanya mbali na mziki, ukitaka kutembelea website ya msanii huyo tembelea 
www.baghdad 255.wordpress.com

I-View Studio kurekodi Video mpya ya Diamond Platnumz


KAMPUNI I-View Studios ya mjini Dar es Salaam imeshinda mchakato wa kurekodi video mpya ya msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambayo usaili wake utafanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, Dar es Salaam.
Akizungumza mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema I-View imepata nafasi hiyo kutokana na kiwango kikubwa cha video kadhaa ilizofanya lakini pia vifaa ilivyo navyo na uwezo wa wafanyakazi wake.
“Siku zote kila mtu anaangalia kitu kizuri, Diamond ametaka kufanya mapinduzi katika tasnia ya muziki, lakini kufanya mapinduzi kunahusisha vitu vingi, tungo zake yeye kama msanii, studio anayorekodia watu watakaoshiriki kwenye video yake kampuni itakayorekodi video pia, lakini mwisho wa siku I-View chini ya Raqey Mohamed ndio imeshinda nafasi hiyo.
“Raqey anafahamika kwa kazi zake pamoja na kurekodi matangazo mbalimbali ya Televisheni, picha mnato lakini pia video za wasanii Taznim ya Kwasakwasa, Utanikumbuka ya Suma Lee ni baadhi ya kazi ambazo zinaonyesha uwezo alionao lakini pia Diamond na timu yake tumeweza kuona vifaa vipya na vya kisasa ambavyo Raqey anavyo kwa sasa na hakuna kwa Afrika Mashariki na Kati,” alisema.
Kwa upande wake Raqey ambaye ni Mkurugenzi wa I-View alisema anahitaji kuifanya kazi hiyo kuwa tofauti ili kusukuma mbele sekta ya mawasiliano na muziki kwa ujumla.
“Sisi kama I-View tunafurahi kufanya kazi na Diamond, ni msanii mzuri na mkubwa ambaye kazi zake zinaonekana, hatutamuangusha na mashabiki na wasanii wengine wasubirie kazi itakapotoka,” alisema.
I-View pia watashiriki katika mchakato wa kupata watu watakaonekana kwenye video hiyo ambayo ni kwa mara ya kwanza nchini kutafanywa usaili wa washiriki. Usaili huo utafanyika Jumamosi katika ukumbi wa Nyumbani Lounge ambao unamilikiwa na mwanamuziki Lady Jaydee. Majina ya majaji wataochuja yatanatarajiwa kutangazwa leo.

PICHA MBALIMBALI ZA SERENGETI FIESTA 2012 MOROGORO....





B12 & PQ
PQ & ROMY JONS
B12,PQ & ROMY
Romy Jons tayari kwenye mashine.....
Bepali la Kihaya ndani ya mjengo....

Mpoki akimnadi Wema kwa mashabiki.....
Wema akijiandaa kutoa burudani....
JB & WEMA
Ray akimtamburisha Jb....
JB Akiwapa raha mashabiki....
Licha ya kuwa na kitambi ila kwenye mauno weeeeeeh!
Anapiga hadi Danadana.....
Ray....
Akijiandaa kusakata rumba....
Mauno yanaruhusiwa pia....

Mashabiki wakigombania Shati la Ray zaidi ya dakika 20....
Mmmmmh! Hata Super Nyamwera na Mandela hawafui dafu....
AT...
Dimpoz....
Rich Mavoko
Ben Pol
Dayna