DIAMOND
AKIONGEA......Tarehe 10 ya mwezi wa 11 siku ya juma mosi ni moja ya siku ambazo
sitozisahau maishani mwangu.
Baada
ya kumaliza majukumu yangu ya kila siku, nilikwenda masaki kumwona mmoja wa
jamaa zangu wa karibu nikiwa na Blogger wangu Bestizzo pamoja na mwanafamilkia
ya wasafi Dumi(Dancer) Mishale ya saa moja hivi nikiwa maeneo ya masaki karibu
na kona ya msasani nilipata ajali ambayo haikuwa kubwa sana ingawa imesababisha
uharibifu kwa kiasi kikubwa, Kama mjuavyo barabara ya msasani ni ndogo na gari
huwa haziko katika mwendo wa kasi... ghafla dereva wa pikipiki alikatisha mbele
yangu na katika kujaribu kumkwepa nikagonga gari ndogo aina ya Rav 4 ambapo
ilisababisha dereva wa pikipiki kuanguka katikati ya gari zote mbili. Hiyo ndio
hali halisi ya ajali niliyokutana nayo jumamosi iliyopita.
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutunusuru wote bila majeraha makubwa zaidi ya maumivu tu ya hapa na pale.
Hii ni pikipiki ambayo ni chanzo cha ajali.....
|