Huku Manchester United wakionekana kujiandaa kutangaza usajili wa
kiungo mshambuliaji Pedro Rodriguez , mahasimu wao toka jijini
Manchester Man City wameingilia kati usajili huo na kutishia nafasi ya
United.
City kupitia kwa mkurugenzi wake mtendaji Txiki Bergistan wanajiandaa
kupeleka ofa ya euro milioni 30 kwa ajili ya mchezaji huyo ambapo
inaelezwa kuwa ofa yao inazidi ofa ya United kwa euro milioni 4 ambapo
United wametoa ofa ya euro milioni 26.
United kwa siku za hivi karibuni wamekuwa wakitajwa kuwa karibu
kumsajili mchezaji huyu ambaye ni dhahiri hana nafasi ya kuumu kwenye
kikosi cha kwanza cha Barcelona na ameweka wazi azma yake ya kutaka
kuondoka.
Manchester City wanaonekana kutumia faida ya ukaribu ulioko kati ya
wakurugenzi wake wawili Txiki Bergistan na Feran Soriano na klabu ya
Barcelona ambapo wawili hao waliwahi kufanya kufanya kazi kwa miaka
mingi kwenye klabu hii ya huko Catalunya .
Hata hivyo bado ofay a Manchester City haijawasilishwa rasmi kwa
Barcelona na hadi sasa mazungumzo rasmi ambayo yamefanyika ni kati ya
Barca na United na inaweza kufikia hatua ya mchezaji mwenyewe kuchagua
mahali anakotaka kwenda .