AJE AJE WAKUBWA NA WADOGO WENZA ....!!!!!!!!!!
SHUKRANI...kwa wote ambao mme weza kuitembelea blog hii ya darls babie ...na sina kubwa lakuw lipa
kuwaombea kwa mungu muendelee kuwa na moyo kama huo na sio kwangu tuu hadi sehemu mbali mbali mie naamini katika maisha watu utoka kwa njia nyingi tuu nausitegeemee sehemu moja jipange muombe mungu wakoo ata weza kuku saidia kufikia malengo yako unayo yaitaji sina mengi ya kusema wadau wangu zaidi tu ya kuwatakia maisha mema yenye furaha naamani ......natusi msahau mungu wetu tutambue kuwa duniani tuna pita sio maisha ya milele so yatu pasa tujipange vyema tana kwakiukamilifu ili tuweze kupambana na shida na raha pia zijazoo mbele yetushukrani by darls babie,,, NIKI ONGOZWA NA ASURAS TECHNOLOGIES
kuwaombea kwa mungu muendelee kuwa na moyo kama huo na sio kwangu tuu hadi sehemu mbali mbali mie naamini katika maisha watu utoka kwa njia nyingi tuu nausitegeemee sehemu moja jipange muombe mungu wakoo ata weza kuku saidia kufikia malengo yako unayo yaitaji sina mengi ya kusema wadau wangu zaidi tu ya kuwatakia maisha mema yenye furaha naamani ......natusi msahau mungu wetu tutambue kuwa duniani tuna pita sio maisha ya milele so yatu pasa tujipange vyema tana kwakiukamilifu ili tuweze kupambana na shida na raha pia zijazoo mbele yetushukrani by darls babie,,, NIKI ONGOZWA NA ASURAS TECHNOLOGIES
SIMBA KUKIPIGA NA TIMU YA OLIECH JUMAMOSI
Simba SC
KATIKA kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii, mabingwa wa Tanzania Bara,
Simba SC, Jumamosi watacheza mechi ya kujipima nguvu na Mathare United
ya Kenya kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.
Habari za ndani kutoka Simba, ambazo zimepatikana, zimesema kwamba
tayari makubaliano yamefikiwa na timu timu hiyo ya Daraja la Kwanza
Kenya, ambayo ilimuibua kisoka mshambuliaji wa AJ Auxerre ya Ufaransa,
Dennis Oliech.
Simba itamenyana na Azam katika mechi ya Ngao ya Jamii ya kuashiria
kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Septemba 8,
mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Habari za ndani kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimesema
kwamba, kuchelewa kwa mechi hiyo ambako kumeenda sambamba na kuchelewa
kuanza kwa ligi hiyo, kumetokana na kuchelewa kufikiwa mwafaka mapema wa
mkataba mpya wa udhamini wa Ligi Kuu.
Mkataba wa awali wa Vodacom na TFF unafikia tamati mwishoni mwa mwezi
huu na kusainiwa mkataba mwingine, baada ya majadiliano yanayoendelea.
Lakini kwa kuwa Mkutano Mkuu wa TFF uliopita uliridhia kuanzia msimu
ujao Ligi Kuu iendeshwe na kampuni itakayoundwa na klabu za Ligi Kuu
mjadala kuhusu udhamini mpya wa ligi umekuwa mrefu kutokana na kuhusisha
pande tatu, klabu, wadhamini na shirikisho.
Lakini sasa, kwa vyovyote, hata maridhiano ya mkataba mpya wa udhamini
na Vodacom yachelewe tena, mechi hiyo itachezwa Septemba 8, ikiwa ni
wiki moja kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.
Kihistoria hiyo itakuwa mechi ya tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini
na ya pili kuishirikisha timu nje ya wapinzani wa jadi wa soka ya
Tanzania, Simba na Yanga.
Mtibwa ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na ikashinda
mabao 2-1 na kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu ya
Tanzania ikiwa bado inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
kupitia bia ya Safari Lager, ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao
kihistoria.
Katika mechi hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na mwaka
juzi Yanga iliifunga tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na
mwaka jana, Simba ilitwaa Ngao ya kwanza katika historia yake, kwa
kuifunga Yanga mabao 2-0.
MISS ILALA NI TAR 7 SEPTEMBER 2012
warimbwende hao wa pande za ilala
tarehe 30 august 2012 siku ya alhamisi , kutakuwa na mashindano ya vipaji kabla ku mpata
malkia ambae nata vikwa taji la mlimbwendae wa ilala
HIVI NDIVYO WASHINDI WA BIBI BOMBA WALIVYOKUA WAKIJINYAKULIA ZAWADI ZAO
SHINDANO la <Bibi Bomba> lilikuwa likiratibiwa na kituo cha
Clouds TV, usiku wa kuamkia leo limefikia tamati na Veronica Mpangala
akiibuka mshindi wa kitita cha 5,000, 000/= (milioni tano) nafasi
ya pili ilichukuliwa na Anna Saidi ambaye alijipatia kiasi cha shilingi
milioni tatu, na mshindi namba tatu alikuwa ni Nasra Mohamed ambaye alijipatia kiasi cha shilingi milioni moja na nusu.
Subscribe to:
Posts (Atom)