Maajabu Tembea uone: hizi ni barabara nyingine 5 hatari duniani… utaendesha gari hapa?


 Ni dunia na ilivyoumbwa, kuna sehemu ambazo hatujawahi au hatutofika kabisa lakini teknolojia imeturahisishia na kutupa nafasi ya kuona kukojekukoje ambapo hii ya barabara nayo nilikua siijui, tazama list ya barabara zenyewe kwenye picha na hiyo video hapo chini baada ya picha.





Iphone 7 inakaribia kutoka… Designers wamejitengenezea hizi.

Kampuni maarufu duniani ya Apple ambayo imekua ikitoa bidhaa mbalimbali zikiwemo simu za mkononi za Iphone inatarajia kutoa na kulionyesha toleo jipya la simu za Iphone 7 September 2015 lakini mpaka sasa hivi kuna designers wameanza kujaribu kuitengenezea picha itatokaje.




Forget LUPITA NYONG’O’s fake dress… see CORAZON wearing a $1 million dress

 According to Corazon Kwamboka, the dress she is wearing in the photo below is worth 1 million USD and her boyfriend will be buying it for her.

Check it out;

Million dollar dress by @smfashionhouse. OMG! The detail in this dress is crazy Swarovski stones etc, this is why a girl finna grind to be able to buy nice things. Anyway, thank God my boyfriend is getting it fi mi. He calls me #brokepikin

Mtoto wa ajabu azaliwa Hospitali ya Mkoa Shinyanga

Maskini Huyu mtoto amezaliwa usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya serikali ya Shinyanga akiwa na Vingo sehemu zisizo sahihi na baada ya muda alifariki Dunia

Najiuliza kwa Sauti Je nini Sababu za Watoto Kama Hawa ? Kwani matukio ya wazazi kujifungua watoto wa ajabu yamekuwa mengi nyakati hizi....

Bunge Lamkingia Kifua Zitto Kabwe......Lasema Bado ni Mbunge Halali na Spika wa Bunge ana Mamlaka Kisheria Ya Kutengua Maamuzi ya CHADEMA


Ofisi ya Bunge imesema haijapata barua yoyote kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema).

Kauli ya hiyo ya Bunge imekuja siku moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutangaza kumvua uanachama Zitto, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa
Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alisema kutokana na hali hiyo, Zitto bado ni mbunge halali wa Kigoma Kaskazini na kwamba anapaswa kuendelea na shughuli zake kwa mujibu wa sheria.
Dk Thomas Kashililah, amebainisha kuwa endapo Bunge litapata taarifa rasmi ya Chadema kumvua uanachama Zitto, lazima Bunge hilo lifanye kwanza uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili ndipo litoe uamuzi.
Pia amesema sakata la mbunge wa Bunge hilo kuvuliwa uanachama na chama chake si la kwanza, kwani tayari kuna mbunge aliyevuliwa uanachama na chama chake lakini Bunge hilo halikumvua uanachama wake baada ya kumaliza uchunguzi wake. Hata hivyo hakumtaja mbunge huyo.
“Utaratibu ulivyo, chama huliandikia Bunge kuhusu kumvua uanachama mbunge na Bunge kabla ya uamuzi wowote hufuatilia kwanza sababu za kuvuliwa uanachama huo, ili kujiridhisha kama zilikuwa halali au la,” alisema Kashililah.
Alisema baada ya hapo Bunge hilo huwasiliana na Msajili wa Vyama vya Siasa ili ofisi hiyo ya msajili iweze kupitia Katiba ya chama husika na kupitia sababu za chama husika zinazoweza kumvua uanachama mwanachama wake na kama kweli zimekiukwa.
“Baada ya suala hilo kupelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa, Spika wa Bunge, hutoa uamuzi baada ya kuchunguza na uamuzi huo, hupelekwa kwa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) kwa ajili ya kufanyiwa kazi zaidi,”alisisitiza.
Aidha alisisitiza: “Si lazima Spika akubaliane na uamuzi wa kutengua ubunge wa mbunge husika kwani kama haikuwa halali kwa mbunge huyo kuvuliwa uanachama, Spika hubatilisha uamuzi wake wa kumvua ubunge mhusika,” alisema.
Alisema Spika Anne Makinda katika kipindi chake alishawahi kutoa uamuzi wa kubatilisha mbunge fulani kuvuliwa ubunge hata baada ya chama chake kumvua uanachama.
Akizungumzia suala hilo, Zitto, alisema kwa upande wake bado ni mbunge na anaendelea na kazi yake ya Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) hadi pale atakapopatiwa taarifa rasmi ya kuvuliwa uanachama na ubunge wake.
“Naendelea na kazi kama vile hakuna kilichotokea, sina taarifa yoyote ya kuvuliwa uanachama wangu wala ubunge, habari hizi nimezisikia kwenye vyombo vya habari, sijaitwa na Mahakama kuambiwa kinachoendelea,”alisema Zitto.
Alisema kwa sasa anaendelea kuongoza kamati hiyo na jana alikutana na menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), leo kamati yake inatarajia kukutana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), pia watakutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mwanasheria Mkuu kuhusu mapato ya akaunti za madini.
Aidha alisema pamoja na kuendelea kama kawaida na shughuli zake za kibunge bungeni, pia anatarajia kesho kwenda Kigoma kwa ajili ya shughuli za maendeleo jimboni kwake, kabla ya kuhudhuria vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kuanza rasmi Machi 17, mwaka huu.
Alisema kwa upande wake, anachukulia suala hilo kama changamoto ambayo inazidi kumkuza na kumkomaza katika medani za siasa nchini na duniani kote.
Kwa upande wake, Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema chama hicho kinajitahidi kulifanyia kazi suala hilo kwa kuzingatia sheria na taratibu zote, ikiwemo kuandaa na kuiwasilisha wakati wowote barua inayomvua uanachama Zitto, ili suala hilo lifanyiwe uamuzi mapema.
“Kwa sasa suala hili la Zitto limewaingia Watanzania wengi, sasa sisi tunataka tulifanyie kazi mapema, ili uamuzi ufanywe mapema na suala hili liishe. Kuna mambo mengi ya maana yanahitaji kujadiliwa kitaifa kama vile masuala ya uandikishaji katika Daftari la Wapiga kura kwa mfumo wa BVR,” alisema.
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ambaye juzi alitangaza kuwa chama hicho kimemvua uanachama mbunge huyo, jana alimwambia mwandishi kuwa, jopo la wanasheria wa chama hicho litaifikisha taarifa ya Zitto kuvuliwa uanachama kwa Kamati Kuu ya chama ifikapo Mei, mwaka huu.
Alisema, "Kutokana na utaratibu uliopangwa wa Kamati Kuu kukutana kila baada ya miezi mitatu, suala la Zitto litasubiri kikao kingine cha kawaida cha kamati hiyo kitakachokaa mwezi Mei. Kikao kilichopita kilikaa Februari mwaka huu".
Kwa maelezo ya Lissu, baada ya hapo ndipo wataiandikia barua Tume ya Uchaguzi (NEC) kuijulisha kuwa Zitto si mwanachama wa chama hicho tena au la.

Ombi Hili la Wema Sepetu, Likufikiae na Wewe….Tubadilike

“Watanzania wenzangu, naombeni leo tujiulize: mitandao ya kijamii ina kazi gani kama sio kuelimisha, kuendeleza na kunufaisha jamii?

Huu ni mwaka 2015. Kama kupendana bure, tushapendana vya kutosha. Kama kutukanana bila sababu, tushatukanana vya kutosha. Kama kushabikia vitu ambavyo havina msaada wowote kwa sisi na familia zetu, tushashabikia vya
kutosha.

Imefika hatua ya kunyanyuana, sio kushushana. Kuelimishana, sio kusemana. Kupeana moyo, sio kukatishana tamaa.

Imefika hatua ya kutegemea mabadiliko, na kupigania mabadiliko.

Nakuomba wewe kaka angu, dada angu, mama angu, baba angu...nakuomba ufanye maamuzi leo, kwamba kesho yako haitakua kama jana yako.

Kwa jina naitwa Wema Sepetu. Na leo hii nimeamua kwamba kesho yangu, haitakua kama jana yangu!

Wewe je? “.-Wema  mwenye followers zaidi ya laki nne mtandaoni ameandika haya na kuungwa mkono na mashabiki wengi na hata wale wanomdisi.

Asante sana Wema, ujumbe umefika.

Kwa jina naitwa Mzee wa Ubuyu  na leo hii nimeamua kesho yangu haitakauwa kama jana yangu.

11.03.2015 -  Tags:  WEMA

Maneno Haya ya Lulu ,Yachukulie Kama Changamoto

Mrembo na staa wa Bongo Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram ameandika ujumbe  mzuri ambao  kiukweli unaweza kukupa nguvu zaidi kufikia malengo yako kama mtu unaejitambua.

 “The more they try to slow you down on the road of purpose, the faster you have to go..!
You only meet opposition when you're going the
right way”

Kwa tafsiri isiyo rasmi anasema “kwa jinsi wanavyozidi kujaribu kukurudisha nyuma katika njia ya mafanikio ndio inakubidi uongeze mwendo…..na utapingigwa tu pale unapokwenda njia sahii”.

Kwa upande wangu, huu ni ujumbe mzuri sana ambao ningependa niulete hapa  kwenu wadau ili nanyinyi muuchukue kama changamoto ya kufanyikisha mambo yako.

Asante sana Lulu kwa maneno haya mazuri.

Mzee wa Ubuyu

Majina ya Abiria Wote Waliokuwa Katika Ajali iliyouwa Watu Iiringa Jana

Ni ajali ambayo haijawahi kutokea katika maeneo haya," ni baadhi ya maneno yaliyosikika kutoka kwa wakazi wengi wa mjini Mafinga na vitongoji vyake, ambao jana walishuhudia ajali  katika historia ya mji huo.
Ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Scania namba T 689 APJ, mali ya Cipex Company lililokuwa likiendeshwa na Maka Sebastian (26)  na basi aina ya Scania namba T438 CED, mali ya kampuni ya Majinja lililokuwa likiendeshwa na Baraka Gabriel (38).
Wakati lori lilikuwa likielekea Barabara ya Mafinga-Mbeya, basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam.
Ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 42 wakiwemo 40 waliokuwemo katika basi na
wawili katika lori hilo, ilitokea katika eneo la Changarawe takribani kilometa 5 kutoka mjini Mafinga, mkoani Iringa, katika barabara kuu ya Mafinga-Mbeya.
Kati ya waliokufa yupo dereva wa basi hilo, huku dereva wa lori akijeruhiwa vibaya baada ya kuchomwa na kitu kama nondo shingoni mwake.
Akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Asas na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, Mungi alisema ajali hiyo ilitokea jana asubuhi saa tatu na nusu.
Kamanda Mungi alisema jeshi lake kwa kushirikiana na hospitali za Mafinga na Mkoa wa Iringa wanaendelea kutambua majina ya watu waliokufa na  majeruhi.
Kamanda Mungi alisema taarifa zao za awali zinaonesha chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa barabara. Mungi alisema lori na basi hilo yaligongana uso kwa uso wakati madereva wake wakishindana kuwahi kuchepuka moja kati ya mashimo makubwa yaliyopo pembezoni na katikati mwa barabara hiyo katika eneo hilo.
Baadhi ya watu waliotajwa kuwepo katika basi na lori hilo ambao hata hivyo hawakuweza kufahamika mara moja, nani kafa na nani kajeruhiwa ni pamoja na Ester Emanuel, Lusekelo Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni na Frank Chiwango.
Wengine ni Luteni Sanga, Teresia Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine, Mbamba Ipyana, Catherine, Mwajengo, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala, Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin Haule na Dominick Mashauri.
Wengine ni Ester Willy, Lucy Mtenga, Erick Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula, Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi, Upendo William, Charles Lusenge, Neto Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa Iman Mahenge na Juma Sindu.
Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na Oswald.
Habari kutoka Mbeya zinaeleza kuwa wakati basi hilo linaondoka kituoni abiria waliokuwepo kwenye basi hilo walikuwa ni 37 ambao ni: 
Baraka Ndone  ambaye ni dereva, Yahya  Hassan ambaye ni kondakta, Esther    Emmanuel, Henry Lugano, Lusekelo Enock, Jeremia  Watson, Hamad, Olga Solomon, Neto, Theresia Kaminyoge, Frank Chiwanga, Luteni Sanga, Alfred Sanga, Doto Katunga,  Juliana Bukuku, Esther Fidel,  Paulina Josia.
Wengine ni Iman Mahenge,  Catherine Mwate, Mathias Justine,  Rebeka Kasambala,  Upendo William, Mbamba Ipyana,  Ndulile Kasambala, Dk A. Shitindi, Six Erick, Frank Mbaule, Mustafa Ramadhani,  Musa, Omega Mwakasege, Shadra Msigwa, Lucy Mtanga, Charles Mweisonga, Martin Haule, Dominick Mashauri, Kelvin Ebadi, Juma Saidi,  na Nicko