Marehemu Mzee James Bukumbi enzi za uhai wake.
MKURUGENZI
Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Bw. Eric Shigongo, anasikitika
kutangaza kifo cha baba yake mzazi na Mwenyekiti wa Global Publishers
Ltd, Mzee James Bukumbi, kilichotokea usiku wa kuamkia Jumapili Tarehe
26/8/2012 katika Hospitali ya Burhani jijini Dar es salaam.
Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwake Kijitonyama, Barabara ya Sayansi, jirani na Heko Motel, Dar es salaam.
Marehemu
atasafirishwa kwenda Mwanza kwa mazishi Jumanne 28/8/2012 na maziko
yatafanyika kijijini kwake Bupandwamhela, Sengerema, Mwanza.
Habari
ziwafikie ndugu wote wa ukoo wa Bukumbi popote walipo, ndugu wa ukoo
wote wa Kapera popote walipo, wananchi wote wa Jimbo la Buchosa, ndugu,
jamaa na marafiki wa Shigongo popote walipo.