NYANGUMI AFNYA UHARIBIFU WA BOTI NA PIA KUJERUHI WATU

Watu watatu wamejeruhiwa baada ya Nyangumi kuibuka ghafla na kurukia boti waliyokua wakisafiria huko Eastern Cape Afrika Kusini.
Boti ilikua inakwenda polepole ghafla Nyangumi akajitokeza toka chini ya maji na kurukia hiyo boti, waliojeruhiwa ambao baadae kidogo waliokolewa na kikosi cha uokoaji ni mzee wa miaka 41 na abiria wengine wenye umri wa miaka 25 na mwingine 35.

RIHHANA KUFANYA NGOMA NA CHRIS BROWN ITAYO KUWA HEWANI IVI KARIBUNUI KAATAYARI..

 

SHEHE SORANGA AJERUHIWA KWA KUMWAGIWA TINDIKALI.. ZANZIBAR


Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akitolewa katika Chumba cha Huduma ya Mwanzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akipandishwa kwenye Gari ya Wagonjwa kwa lengo la kuwahishwa katika Hospitali ya Muhimbili Dare es Salaam baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
Wananchi mbalimbali wakishuhudia Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akiwahishwa katika Hospitali ya Muhimbili Dare es Salaam baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe. Picha, Maelezo