NIMEJITOA MTANASHATI KWASABABU BOSS ANAPENDA SIFA : SUMA MNAZARETI



Ikiwa ni mda mfupi sana tangu alipoingia katika kampuni yenye wasanii kama Dogo janja, Amazon PNC na wengineo  inayojulikana kama watanashati, Suma Mnazareti ameaschana na chama hilo linaloongozwa na ashati Ostaz Juma Namusoma.

"Nimeamua kujitoa mtanashati, na sababu kubwa katika zote ya kujitoa ni kwamba nilifata kazi kwa Ostaz na sio hela zake, so nilichokuwa nadhania ntakipata mtanashati hakipo,Boss anatafta zaidi sifa na ustaa Tanzania na mimi mziki ni kazi yangu..anaweza akagawa mamilioni kwa watu ili atajwe lakini anashindwa kulipa hela ya maana kwa ajili ya video, matokeo yake anatoa shilingi laki tatu? unadhani tutaweza kushindana na video kama za kina Ay za million 30?. nimeuza mpaka balackberry yangu kuongeza kwenye pesa za kukamilisha video yangu, wakati hata nilivyokua ha hustle mwenyewe sikuwahi kuuza sim yangu. so nimejiondoa maana sioni faida yoyote, na mimi mziki kwangu ni kazi nataka nifike mbele zaidi. aliongea Suma

MISS TANZANIA 2000 ATEGEMEA MTOTO SIKU KADHAA SIJAZO

  msanii na ni miss tanzania mwaka 2000 yuko karibuni kuitwa mama  ambae jina lake kamili nii JACQUELINE  NTUYABALIWE anategemea kupata mtoto mungu amjalie salama ajifungue bila matatizo.

MAMBO YALIENDELEA KAMA HIVI NDANI YA FIESTA MOSHI

                                                               recho akitumbuiza
                                                       FA ndani ya nyumba
                           ray the greatest bro akionyesha manjonjo pamoja na ma queen wa bongo movie
                                         DJ zero akisongesha ngoma
                                 watu walifurika sio mchezo big up sana fanz
                                                   raythe greatest pamoja na nyerere
                                            haya sasa wema jiachie mdada na nyerere
                                                         


TAMASHA LA SERENGETI FIESTA LAZINDULIWA MKOANI KILIMANJARO

  Usiku wa Ijumaa utabaki kukumbukwa kwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro kutokana na uzinduzi wa aina yake wa tamasha la 11 la Serengeti Fiesta lillilofana mkoani hapa.

Tanzania Daima ambayo ilikuwepo katika eneo la tukio hilo ilishuhudia mamia ya vijana wakiwa wamejitokea kwa wingi katika uzinduzi huo wa aina yake.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama aliwahamasisha mamia ya mashabiki na wadau mbalimbali waliofika katika uzinduzi huouliofanyika katika Viwanja vya Chuo Cha Ushirika kushrehekea kwa amani na utulivu pamoja na kutosahau kujitokeza katika zoezi la sensa.

Baaadhi ya wasanii waliofunika katika uzinduzi huo ni Shetta , Richie Mavoco, Makomando, Linah, Joh Makini, Mwana Fa bila ya kumsaha mwanamuziki wa kimataifa ambaye pia alikuwa mshindi wa pili katika shindano la Big Brother 2012 Prezzo kutoka nchini kenya.

Wakati huohuo uzinduzi huo ulinogeshwa nawasanii wa nyota wa filamu nchini ambao ni Aunt Ezekiel, Ray Kigosi ‘Ray’, Mwenyekiti wa Bongo Movie Jacob Steven ‘JB’, Steve Nyerere na Wema Sepetu ambao walikuwepo katika uzinduzi wakiwa ambapo walikuwa katika msafara huo kwa minajili ya kusaka vipaji vya kucheza filamu kwa wakaazi wa mkoani hapa.Wasanii hao ambao walitambulishwa jukwaani

Pia waliweza kuonesha namna wanavyoweza kunengua mbali ya kucheza filamu huku mashabiki wakimpigia kelele Wema atingishe nyonga zake mara kadhaa nay eye alifanya hivyo na kushangiliwa ipasavyo.

Tamasha hilo limeandaliwa na Kampuni ya Prime Time Promotions ambayo ni Kampuni dada na Clouds Media Group yenye maskani yake jijini Dar es Salaam.

Wasanii wengine walio onesha uwezo wao katika uzinduzi huo ni pamoja na Juma Kassim ‘Nature’, Ferooz, Stamina, Tash &Juru, Mr. Nice, Recho, Jambo Squard, Rich Mavocal, Ommy Dimpoz, Godzilla na Bob Junior. Jumapili usiku  Agosti 26 tamasha hili litarindima ndani ya uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga.

Bongo Movie washine kwenye Fiesta Moshi......

Jacob Steven "JB" Akiwa kwenye Interview na Millard Ayo wa Cloudz Fm

                                   ndani nya pozi aunt& wema sepeu ndani ya fiesta ya jijini moshi
                                                        Wema akiwa kwenye Interview......
                                        Wema,Steve Nyerere kati na pembeni ni Aunt Ezekiel
                                         Aunt,Ray,Wema,Hartman na Steven Nyerere......
                                mpango mzima wa kuchat tena kitu cha BBM bwana