CHOZI LA RIHANNA LADONDOKA KWENYE MAHOJIANO NA OPRAH KISA CHRISS BROWN

  Rihanna akiwa na mgeni wake oprah winfrey
 Mwanamama mkali wa maswali mazito na ya ndani Oprah winfrey amefanya maojiano na rihanna aliyemfuata kwao barbados.rihanna aliulizwa kuhusu kupigwa na chriss brown alikuwa kama ametoneshwa kidonda vile alitokwa na machozi nakusema kusema"IT WAS EMBARRASSING,IT WAS HUMILIATING, I LOST MY BEST FRIEND

Oprah na rihanna kwa gari
oprah akiingia kwa rihanna nyumbani kwao barbados.

GOD ZILA ANA UCHU WAKUPIGA COLLABO NA 50 CENT

Mkali wa miondoko ya hih hop nchini kutoka salasala godzila a.k.a King zila mesema' ndoto yake siku moja ni kuja kufanya ngoma na mkali wa hiphop kutoka marekan 50 cen't. amesema" king zila kila siku uota ndoto hiyo na anaamin ipo siku ndoto yake itakuwa kweli.

SIR ALEX FURGASON anfikilia nini na manchester united...!!!!



Ferguson anafikiria nini na united yake?
NA BARAKA MBOLEMBOLE Sir Alex Ferguson, mpende kocha huyu, lakini pia unaruhusiwa kutompenda. Kama usipoegemea upande wowote wa kishabiki huyu ni mtu Mama yake mzazi atampenda na kumuona mtoto bora. Lakini hiyo inamtambulisha kama mtu 'ngangari' kinoma katika mchezo wa soka kote England na duniani. Rekodi zake zinazungumza zenyewe, na mara nyingi amekuwa akitwaa mataji ya ligi kuu na Ulaya baada ya kuwa na uwezo wa kuibadili timu yake kutoka 'goi goi' na kwenda nayo uwanjani uku akisoma nyakati na kutwaa makombe kwa tamaduni za Ki-manchester United pekee. Mbinu zake ni za kipekee na vikosi vyake ni kama uchawi, ukitazama namna United ilivyoitia presha Manchester City hadi dakika ya mwisho ya City katika ligi kuu msimu uliopita bila shaka utaamini kuhusu haya nayosema. Baada ya msimu wa bila taji na wengi wakidhani United ilikuwa na kikosi dhaifu, Ferguson ameweka imani kubwa kwa wachezaji vijana katika kikosi chake cha msimu, aliwakosa kwa sehemu kubwa ya msimu viungo Tom Cleverly na Anderson, hawa ni viungo vijana ambao tayari wamepevuka kuwa wachezaji wa kikosi cha lwanza, walifanya vyema wakati United iliposhinda mechi tatu ndani ya wiki tatu dhidi ya timu kubwa za London msimu uliopita, United ilizifunga, Tottenham, Arsenal na Chelsea ndani ya wiki tatu ikicheza ugenini. Kuumia kwa vijana hao kulipeleke Michael Carrick na Ryan Giggs kurudishwa katika kikosi cha kwanza kwa haraka, na hata aliporudi Darren Fletcher timu haikuwa bora na wakakumbana na kipigo kitakatifu kutoka kwa City, United ikaanza kuporomoka na kutolewa katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa. Lakini kimaajabu wakati ligi ikiwa imepamba moto na United ikionekana kuongezeka ubora baada ya Paulo Scholes kurejea uwanjani mara baada ya dirisha dogo la usajili, januari kufunguliwa, Scholes akamfanya Carrick kurejesha kiwango kiasi fulani, uku Giggs akitumia uzoefu wake kuzalisha mabao kvoka katikati ya uwanja au upande wa kusho, Antonio Valencia alikuwa ni kama amefunguliwa 'kamba' katika winga ya kulia, alikuwa mpiga pasi bora wa pili katika ligi kuu msimu uliopita japo alikuwa majeruhi kwa nusu msimu. United ikawa juu ya City kwa tofauti ya pointi nane mechi nne kabla ya ligi kumalizika, lakini tofauti ya mabao ikaamua bingwa baada ya United kushindwa kuwa na 'ngome' imara. United ilikabiliwa na majeruhi wengi sana katika msimu ulipita, japo hiyo haiwezi kuwa sababu ya kukosa kwao kutwaa ubingwa,lakini ilichangia. Wakati Rio Ferdinand alipokuwa anaangaika kuwa 'fiti' mlinzi mwenzake Nemanja Vidic alikuwa katika meza ya madaktari akitibiwa matatizo yake ya goti. Bahati mbaya kwa Ferguson ni kwamba, japo, John Evans amekuwa akicheza na wazoefu hao katika ngome kwa miaka sita bado hajajitofautisha na wachezaji wa timu kama Stoke City, huyu ndiye alitakiwa kuziba 'viraka' katika ulinzi wa United msimu uliopita lakni alishindwa. CRISS smalling ni mlinzi bora kwa walio chini ya miaka 24 katika ligi kuu (kwa mtazamo wangu) lakini kinda huyu ana 'mwili wa plastic' ni mtu wa kuumia umia mara kwa mara, lakini anapokuwa 'fiti' hucheza kama Garry Neville akicheza namba mbili na hucheza kama Allesandro Nesta akicheza nafasi ya kati. Ferguson anaamini tayari ana kikosi bora ambacho kinaweza kutwaa mataji makubwa. SHINJI KAGAWA Hidetoshi Nakata alikuwa ni kipenzi sana cha Wajapan, nakumbuka nami niliwahi kununua jezi timu ya taifa ya Japan kwa kiasi cha shillingi elfu sita na mia tano mwaka 2001 na ilikuwa na namba saba imeandikwa Nakata, Nakata alikuwa Mjapan wa kwanza kucheza soka Ulaya na ndani ya mwaka mmoja akafanikiwa kusìnda 'scuddetto' akiwa na ASpOMA. Ferguson alijaribu mara kadhaa kumtwaa Nakata lakini Roma hawakuwa tayari kumuuza. Soka la Nakata likaanza kutawaliwa na majeraha na taratibu akapotea, lakini sasa Wajan watakuwa na matumaini ya kumuona Kagawa akifikia mafanikio ya juu akiwa na United. Tayari ametwaa mara mbili ubingwa wa Bundesliga akiwa na Borrussia Dortmund katika misimu yake miwili barani Ulaya. Amepevuka na huyu ndiye anayatarajiwa kuwafanya Danny Welbeck, Wayne Rooney na Javier Hernandez kufunga mabao, ametua United kwa kazi ya kuchukua mipira kutoka kwa Carrick(ambaye amekabidhiwa timu) na kuipenyeza kwenye 'mashimo'. Mechi ya ufunguzi dhidi ya Everton wikendi hii inaweza ikamsumbua lakini, Kagawa amekuja United kugawa pasi na kufunga mabao.


Usikose kipindi kipya cha X MIX kila JUMATATU hadi IJUMAA ndani ya DTV


GrooveBack - The Return...Jumamosi hii na EID Pili.


MAMBO JAMBO SUMMER JAM ARUSHA

Na mambo Jambo Summer Jam,Concert itayofanyika siku ya Iddi Mosi pale Sheikh Amri Abeid Stadium Arusha from Saa sita mchana hadi jioni na round hii A City is in tha houseeee!!! Bounako, StopaRhymez, Fidovato, WEUSI, TaigaRaiz, Badtaito, J4c, MayC, Veejay, Gfaya, Meccacheka, EffectZero, Gentriez, YungOmega na MirryCandle juu ya stage la kibabe, sound ya kibabe ni buku mbili  tu siku iyo   endelea kuskiza radio yako inayoaminika..93.0 Mambo Jambo Radio

JayGONGA Presents @Hasheemthedream "The DressCODE" AUGUST 2012


BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA MSANII WA HIP HOP NCHINI ROMA AZUNGUMZA NA MASHABIKI WAKE.

NI baada ya msanii wa hip hop roma kupata ajali mbaya akiongea mawili matatu na na mashabiki wake wote wano penda mziki wake nikiwemo darls babie ndani ya mjengo

EXCLUSIVE VIDEO DOGO JANJA FT PNC.....


EXCLUSIVE OFFICAL VIDEO MAKAVU LIVE FT JOSLIN...


EXCLUSIVE VIDEO


FUNS WANGU WANGU WANALALA MIKA VIDEO YANGU SASA NASHOOT UPYA TUNDA MAN....!!!!!!!!!

tunda man amesema kwamba anataka afanye kitu fans wake mlizike ame amua kurudia upya video yake ya DEMU SIO ambayo ili tengenezwa na adamu juma wa visual lab... kwa sasa ame amua kushuti upya na kampuni inayo usika nautengenezaji wa video mbali mbali sinyingne bali ni APEX chini ya usimamizi wa dir pablo.
hapo tunda man akiwa katika pozi mbali mbali katika kustoot video ya DEMU SIO ili kuwalizisha fans wake na waipende zaidi video yake kwa nin bila nyie asinge fika apa alipo
na AM RECORD ili kuwa iko pamoja na bwana tunda ku mpa sapoti ndani ya hyo video yake mpya