SIR ALEX FURGASON anfikilia nini na manchester united...!!!!



Ferguson anafikiria nini na united yake?
NA BARAKA MBOLEMBOLE Sir Alex Ferguson, mpende kocha huyu, lakini pia unaruhusiwa kutompenda. Kama usipoegemea upande wowote wa kishabiki huyu ni mtu Mama yake mzazi atampenda na kumuona mtoto bora. Lakini hiyo inamtambulisha kama mtu 'ngangari' kinoma katika mchezo wa soka kote England na duniani. Rekodi zake zinazungumza zenyewe, na mara nyingi amekuwa akitwaa mataji ya ligi kuu na Ulaya baada ya kuwa na uwezo wa kuibadili timu yake kutoka 'goi goi' na kwenda nayo uwanjani uku akisoma nyakati na kutwaa makombe kwa tamaduni za Ki-manchester United pekee. Mbinu zake ni za kipekee na vikosi vyake ni kama uchawi, ukitazama namna United ilivyoitia presha Manchester City hadi dakika ya mwisho ya City katika ligi kuu msimu uliopita bila shaka utaamini kuhusu haya nayosema. Baada ya msimu wa bila taji na wengi wakidhani United ilikuwa na kikosi dhaifu, Ferguson ameweka imani kubwa kwa wachezaji vijana katika kikosi chake cha msimu, aliwakosa kwa sehemu kubwa ya msimu viungo Tom Cleverly na Anderson, hawa ni viungo vijana ambao tayari wamepevuka kuwa wachezaji wa kikosi cha lwanza, walifanya vyema wakati United iliposhinda mechi tatu ndani ya wiki tatu dhidi ya timu kubwa za London msimu uliopita, United ilizifunga, Tottenham, Arsenal na Chelsea ndani ya wiki tatu ikicheza ugenini. Kuumia kwa vijana hao kulipeleke Michael Carrick na Ryan Giggs kurudishwa katika kikosi cha kwanza kwa haraka, na hata aliporudi Darren Fletcher timu haikuwa bora na wakakumbana na kipigo kitakatifu kutoka kwa City, United ikaanza kuporomoka na kutolewa katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa. Lakini kimaajabu wakati ligi ikiwa imepamba moto na United ikionekana kuongezeka ubora baada ya Paulo Scholes kurejea uwanjani mara baada ya dirisha dogo la usajili, januari kufunguliwa, Scholes akamfanya Carrick kurejesha kiwango kiasi fulani, uku Giggs akitumia uzoefu wake kuzalisha mabao kvoka katikati ya uwanja au upande wa kusho, Antonio Valencia alikuwa ni kama amefunguliwa 'kamba' katika winga ya kulia, alikuwa mpiga pasi bora wa pili katika ligi kuu msimu uliopita japo alikuwa majeruhi kwa nusu msimu. United ikawa juu ya City kwa tofauti ya pointi nane mechi nne kabla ya ligi kumalizika, lakini tofauti ya mabao ikaamua bingwa baada ya United kushindwa kuwa na 'ngome' imara. United ilikabiliwa na majeruhi wengi sana katika msimu ulipita, japo hiyo haiwezi kuwa sababu ya kukosa kwao kutwaa ubingwa,lakini ilichangia. Wakati Rio Ferdinand alipokuwa anaangaika kuwa 'fiti' mlinzi mwenzake Nemanja Vidic alikuwa katika meza ya madaktari akitibiwa matatizo yake ya goti. Bahati mbaya kwa Ferguson ni kwamba, japo, John Evans amekuwa akicheza na wazoefu hao katika ngome kwa miaka sita bado hajajitofautisha na wachezaji wa timu kama Stoke City, huyu ndiye alitakiwa kuziba 'viraka' katika ulinzi wa United msimu uliopita lakni alishindwa. CRISS smalling ni mlinzi bora kwa walio chini ya miaka 24 katika ligi kuu (kwa mtazamo wangu) lakini kinda huyu ana 'mwili wa plastic' ni mtu wa kuumia umia mara kwa mara, lakini anapokuwa 'fiti' hucheza kama Garry Neville akicheza namba mbili na hucheza kama Allesandro Nesta akicheza nafasi ya kati. Ferguson anaamini tayari ana kikosi bora ambacho kinaweza kutwaa mataji makubwa. SHINJI KAGAWA Hidetoshi Nakata alikuwa ni kipenzi sana cha Wajapan, nakumbuka nami niliwahi kununua jezi timu ya taifa ya Japan kwa kiasi cha shillingi elfu sita na mia tano mwaka 2001 na ilikuwa na namba saba imeandikwa Nakata, Nakata alikuwa Mjapan wa kwanza kucheza soka Ulaya na ndani ya mwaka mmoja akafanikiwa kusìnda 'scuddetto' akiwa na ASpOMA. Ferguson alijaribu mara kadhaa kumtwaa Nakata lakini Roma hawakuwa tayari kumuuza. Soka la Nakata likaanza kutawaliwa na majeraha na taratibu akapotea, lakini sasa Wajan watakuwa na matumaini ya kumuona Kagawa akifikia mafanikio ya juu akiwa na United. Tayari ametwaa mara mbili ubingwa wa Bundesliga akiwa na Borrussia Dortmund katika misimu yake miwili barani Ulaya. Amepevuka na huyu ndiye anayatarajiwa kuwafanya Danny Welbeck, Wayne Rooney na Javier Hernandez kufunga mabao, ametua United kwa kazi ya kuchukua mipira kutoka kwa Carrick(ambaye amekabidhiwa timu) na kuipenyeza kwenye 'mashimo'. Mechi ya ufunguzi dhidi ya Everton wikendi hii inaweza ikamsumbua lakini, Kagawa amekuja United kugawa pasi na kufunga mabao.