Orijino
Komedi wakiwa na Vengu wa mwisho kulia, hapa ilikua kabla hajaanza kuugua.
Nafaham ni watanzania wengi ambao wanalo hili swali kama
mimi, toka tulipoacha kumuona msanii/mchekeshaji Vengu kwenye ORIJINO KOMEDI
baada ya kuumwa, zilizuka stori nyingi sana
lakini stori ya mwisho mimi kuipata ni kwamba alisharudi Tanzania akitokea kwenye matibabu India na afya
yake inaendelea vizuri.
Baada ya kufahamu hivyo nikawa na kiu ya kutaka kujua ni
lini tutaanza kumuona akichekesha tena ndani ya Orijino Komedi hivyo nikapata
nafasi ya kuzungumza na Wakuvanga ambae ndio mkurugenzi wa kampuni
inayoisimamia Orijino Komedi.
Namkariri akisema “ukweli niwe muwazi, kwa afya yake na
tatizo alilonalo tunazungumzia tatizo la mshipa wa fahamu, tunazungumzia kitu
kinaitwa ubongo, hayo matatizo yanachukua muda mrefu sana ukizungumza
ukiwaambia watanzania kwamba atarudi hivi karibuni unakua unajidanganya wewe na
watanzania wenzio, ndio maana siku zote tunasema ukiwa na nafasi ya kumuombea
mtu unaempenda muombee, mi siwezi kuahidi kwamba labda atarudi mwezi ujao au
mwaka ujao”
Kuhusu kutafuta mtu wa kuziba nafasi ya Vengu, Wakuvanga amesema
“tutaendelea kuwa na jina la Vengu maisha yote ya Komedi, kwetu sisi iko
tofauti kidogo sisi tumeapa.. ndivyo tunavyoishi, tuko saba mpaka tunakufa..
kuongezeka kwa mtu labda sisi tukae pembeni tuwatafute watu wengine lakini
tutaendelea kuwa saba, hata maeneo tunayoishi na jinsi tunavyoishi mara nyingi
tunaishi tuko saba, akipungua mmoja bado tuko saba”