EXCLUSIVE: HII NDIO KAULI YA MWISHO YA ORIJINO KOMEDI KUHUSU VENGU!
Orijino
Komedi wakiwa na Vengu wa mwisho kulia, hapa ilikua kabla hajaanza kuugua.
Nafaham ni watanzania wengi ambao wanalo hili swali kama
mimi, toka tulipoacha kumuona msanii/mchekeshaji Vengu kwenye ORIJINO KOMEDI
baada ya kuumwa, zilizuka stori nyingi sana
lakini stori ya mwisho mimi kuipata ni kwamba alisharudi Tanzania akitokea kwenye matibabu India na afya
yake inaendelea vizuri.
Baada ya kufahamu hivyo nikawa na kiu ya kutaka kujua ni
lini tutaanza kumuona akichekesha tena ndani ya Orijino Komedi hivyo nikapata
nafasi ya kuzungumza na Wakuvanga ambae ndio mkurugenzi wa kampuni
inayoisimamia Orijino Komedi.
Namkariri akisema “ukweli niwe muwazi, kwa afya yake na
tatizo alilonalo tunazungumzia tatizo la mshipa wa fahamu, tunazungumzia kitu
kinaitwa ubongo, hayo matatizo yanachukua muda mrefu sana ukizungumza
ukiwaambia watanzania kwamba atarudi hivi karibuni unakua unajidanganya wewe na
watanzania wenzio, ndio maana siku zote tunasema ukiwa na nafasi ya kumuombea
mtu unaempenda muombee, mi siwezi kuahidi kwamba labda atarudi mwezi ujao au
mwaka ujao”
Kuhusu kutafuta mtu wa kuziba nafasi ya Vengu, Wakuvanga amesema
“tutaendelea kuwa na jina la Vengu maisha yote ya Komedi, kwetu sisi iko
tofauti kidogo sisi tumeapa.. ndivyo tunavyoishi, tuko saba mpaka tunakufa..
kuongezeka kwa mtu labda sisi tukae pembeni tuwatafute watu wengine lakini
tutaendelea kuwa saba, hata maeneo tunayoishi na jinsi tunavyoishi mara nyingi
tunaishi tuko saba, akipungua mmoja bado tuko saba”
BAGHDAD AVUKA BODA.
Msanii aliezuiliwa kufanya show, kupiga intaview, wala
kolabo ili kupisha muda wa kuanda ngoma ambazo yuko mbioni kuingia both beat
produced by c.e.o wa chofacho rec studio iliyoko marekani ambae ndio
inamsimamia msanii huyo kwa sasa imeamua kufungua website kwa ajili ya kuweka
mambo yanayohusu mziki, maisha na harkati anazozifanya mbali na mziki, ukitaka
kutembelea website ya msanii huyo tembelea
www.baghdad 255.wordpress.com
I-View Studio kurekodi Video mpya ya Diamond Platnumz
KAMPUNI
I-View Studios ya mjini Dar es Salaam imeshinda mchakato wa kurekodi video mpya
ya msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambayo usaili wake utafanyika
Jumamosi kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, Dar es Salaam.
Akizungumza
mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya One Touch Solutions, Petter
Mwendapole alisema I-View imepata nafasi hiyo kutokana na kiwango kikubwa cha
video kadhaa ilizofanya lakini pia vifaa ilivyo navyo na uwezo wa wafanyakazi
wake.
“Siku
zote kila mtu anaangalia kitu kizuri, Diamond ametaka kufanya mapinduzi katika
tasnia ya muziki, lakini kufanya mapinduzi kunahusisha vitu vingi, tungo zake
yeye kama msanii, studio anayorekodia watu watakaoshiriki kwenye video yake
kampuni itakayorekodi video pia, lakini mwisho wa siku I-View chini ya Raqey
Mohamed ndio imeshinda nafasi hiyo.
“Raqey
anafahamika kwa kazi zake pamoja na kurekodi matangazo mbalimbali ya
Televisheni, picha mnato lakini pia video za wasanii Taznim ya Kwasakwasa,
Utanikumbuka ya Suma Lee ni baadhi ya kazi ambazo zinaonyesha uwezo alionao
lakini pia Diamond na timu yake tumeweza kuona vifaa vipya na vya kisasa
ambavyo Raqey anavyo kwa sasa na hakuna kwa Afrika Mashariki na Kati,” alisema.
Kwa
upande wake Raqey ambaye ni Mkurugenzi wa I-View alisema anahitaji kuifanya kazi
hiyo kuwa tofauti ili kusukuma mbele sekta ya mawasiliano na muziki kwa ujumla.
“Sisi
kama I-View tunafurahi kufanya kazi na Diamond, ni msanii mzuri na mkubwa
ambaye kazi zake zinaonekana, hatutamuangusha na mashabiki na wasanii wengine
wasubirie kazi itakapotoka,” alisema.
I-View
pia watashiriki katika mchakato wa kupata watu watakaonekana kwenye video hiyo
ambayo ni kwa mara ya kwanza nchini kutafanywa usaili wa washiriki. Usaili huo
utafanyika Jumamosi katika ukumbi wa Nyumbani Lounge ambao unamilikiwa na
mwanamuziki Lady Jaydee. Majina ya majaji wataochuja yatanatarajiwa kutangazwa
leo.
PICHA MBALIMBALI ZA SERENGETI FIESTA 2012 MOROGORO....
B12 & PQ |
PQ & ROMY JONS |
B12,PQ & ROMY |
Romy Jons tayari kwenye mashine..... |
Bepali la Kihaya ndani ya mjengo.... |
Mpoki akimnadi Wema kwa mashabiki..... |
Wema akijiandaa kutoa burudani.... |
JB & WEMA |
Ray akimtamburisha Jb.... |
JB Akiwapa raha mashabiki.... |
Licha ya kuwa na kitambi ila kwenye mauno weeeeeeh! |
Anapiga hadi Danadana..... |
Ray.... |
Akijiandaa kusakata rumba.... |
Mauno yanaruhusiwa pia.... |
Mashabiki wakigombania Shati la Ray zaidi ya dakika 20.... |
Mmmmmh! Hata Super Nyamwera na Mandela hawafui dafu.... |
![]() |
AT... |
![]() |
Dimpoz.... |
![]() |
Rich Mavoko |
![]() |
Ben Pol |
![]() |
Dayna |
Subscribe to:
Posts (Atom)