USIKOSE KUANGALIA MASHINDANO YA MISS EAST-AFRICA KATIKA M-NET.




Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yataonyeshwa LIVE kupitia Mnet ambapo yanatarajiwa kutuizamwa na watu wanaokadiliwa kufikia million 200 kupitia televison na kwa njia ya internet Dunia nzima.
 Aidha maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea kwa kasi ambapo yamepangwa kufanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City,  jijini Dare s salaam, Tanzania badala ya mwezi September kama ilivyokuwa imetangazwa awali ili kutoa muda zaidi kwa Ncgi ambazo hazijapata wawakilishi wao kuweza kukamilisha zoezi hilo.
 Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake ambapo yatashirikisha warembo kutoka katika Nchi 16 za ukanda wa afrika mashariki.
Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.
 Mashindano ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni wa Afrika mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama Nchi wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika
 Tayari baadhi ya Nchi zinazoshiriki mashindano hayo zimeshatangaza wawakilishi wake ambazo ni Eritrea, Ethiopia, Uganda, Southern Sudan, Malawi na Seychelles. Nchi zilizosalia zinatarajiwa kutangaza wawakilishi wao kabla ya tarehe ya mwisho ambayo ni tarehe 28 mwezi September.
 Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,.
 Rena Callist,
Executive Producer,
MISS EAST AFRICA PAGEANT

NIMEJITOA MTANASHATI KWASABABU BOSS ANAPENDA SIFA : SUMA MNAZARETI



Ikiwa ni mda mfupi sana tangu alipoingia katika kampuni yenye wasanii kama Dogo janja, Amazon PNC na wengineo  inayojulikana kama watanashati, Suma Mnazareti ameaschana na chama hilo linaloongozwa na ashati Ostaz Juma Namusoma.

"Nimeamua kujitoa mtanashati, na sababu kubwa katika zote ya kujitoa ni kwamba nilifata kazi kwa Ostaz na sio hela zake, so nilichokuwa nadhania ntakipata mtanashati hakipo,Boss anatafta zaidi sifa na ustaa Tanzania na mimi mziki ni kazi yangu..anaweza akagawa mamilioni kwa watu ili atajwe lakini anashindwa kulipa hela ya maana kwa ajili ya video, matokeo yake anatoa shilingi laki tatu? unadhani tutaweza kushindana na video kama za kina Ay za million 30?. nimeuza mpaka balackberry yangu kuongeza kwenye pesa za kukamilisha video yangu, wakati hata nilivyokua ha hustle mwenyewe sikuwahi kuuza sim yangu. so nimejiondoa maana sioni faida yoyote, na mimi mziki kwangu ni kazi nataka nifike mbele zaidi. aliongea Suma

MISS TANZANIA 2000 ATEGEMEA MTOTO SIKU KADHAA SIJAZO

  msanii na ni miss tanzania mwaka 2000 yuko karibuni kuitwa mama  ambae jina lake kamili nii JACQUELINE  NTUYABALIWE anategemea kupata mtoto mungu amjalie salama ajifungue bila matatizo.

MAMBO YALIENDELEA KAMA HIVI NDANI YA FIESTA MOSHI

                                                               recho akitumbuiza
                                                       FA ndani ya nyumba
                           ray the greatest bro akionyesha manjonjo pamoja na ma queen wa bongo movie
                                         DJ zero akisongesha ngoma
                                 watu walifurika sio mchezo big up sana fanz
                                                   raythe greatest pamoja na nyerere
                                            haya sasa wema jiachie mdada na nyerere
                                                         


TAMASHA LA SERENGETI FIESTA LAZINDULIWA MKOANI KILIMANJARO

  Usiku wa Ijumaa utabaki kukumbukwa kwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro kutokana na uzinduzi wa aina yake wa tamasha la 11 la Serengeti Fiesta lillilofana mkoani hapa.

Tanzania Daima ambayo ilikuwepo katika eneo la tukio hilo ilishuhudia mamia ya vijana wakiwa wamejitokea kwa wingi katika uzinduzi huo wa aina yake.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama aliwahamasisha mamia ya mashabiki na wadau mbalimbali waliofika katika uzinduzi huouliofanyika katika Viwanja vya Chuo Cha Ushirika kushrehekea kwa amani na utulivu pamoja na kutosahau kujitokeza katika zoezi la sensa.

Baaadhi ya wasanii waliofunika katika uzinduzi huo ni Shetta , Richie Mavoco, Makomando, Linah, Joh Makini, Mwana Fa bila ya kumsaha mwanamuziki wa kimataifa ambaye pia alikuwa mshindi wa pili katika shindano la Big Brother 2012 Prezzo kutoka nchini kenya.

Wakati huohuo uzinduzi huo ulinogeshwa nawasanii wa nyota wa filamu nchini ambao ni Aunt Ezekiel, Ray Kigosi ‘Ray’, Mwenyekiti wa Bongo Movie Jacob Steven ‘JB’, Steve Nyerere na Wema Sepetu ambao walikuwepo katika uzinduzi wakiwa ambapo walikuwa katika msafara huo kwa minajili ya kusaka vipaji vya kucheza filamu kwa wakaazi wa mkoani hapa.Wasanii hao ambao walitambulishwa jukwaani

Pia waliweza kuonesha namna wanavyoweza kunengua mbali ya kucheza filamu huku mashabiki wakimpigia kelele Wema atingishe nyonga zake mara kadhaa nay eye alifanya hivyo na kushangiliwa ipasavyo.

Tamasha hilo limeandaliwa na Kampuni ya Prime Time Promotions ambayo ni Kampuni dada na Clouds Media Group yenye maskani yake jijini Dar es Salaam.

Wasanii wengine walio onesha uwezo wao katika uzinduzi huo ni pamoja na Juma Kassim ‘Nature’, Ferooz, Stamina, Tash &Juru, Mr. Nice, Recho, Jambo Squard, Rich Mavocal, Ommy Dimpoz, Godzilla na Bob Junior. Jumapili usiku  Agosti 26 tamasha hili litarindima ndani ya uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga.

Bongo Movie washine kwenye Fiesta Moshi......

Jacob Steven "JB" Akiwa kwenye Interview na Millard Ayo wa Cloudz Fm

                                   ndani nya pozi aunt& wema sepeu ndani ya fiesta ya jijini moshi
                                                        Wema akiwa kwenye Interview......
                                        Wema,Steve Nyerere kati na pembeni ni Aunt Ezekiel
                                         Aunt,Ray,Wema,Hartman na Steven Nyerere......
                                mpango mzima wa kuchat tena kitu cha BBM bwana

NEW TRACK: KONTAGOUS - Kama Laana


AJE AJE WAKUBWA NA WADOGO WENZA ....!!!!!!!!!!

SHUKRANI...kwa wote ambao mme weza kuitembelea blog hii ya darls babie ...na sina kubwa lakuw lipa
kuwaombea kwa mungu muendelee kuwa na moyo kama huo na sio kwangu tuu hadi sehemu mbali mbali mie naamini katika maisha watu utoka kwa njia nyingi tuu nausitegeemee sehemu moja jipange muombe mungu wakoo ata weza kuku saidia kufikia malengo yako unayo yaitaji sina mengi ya kusema wadau wangu zaidi tu ya kuwatakia maisha mema yenye furaha naamani ......natusi msahau mungu wetu tutambue kuwa duniani tuna pita sio maisha ya milele so yatu pasa tujipange vyema tana kwakiukamilifu ili tuweze kupambana na shida na raha pia zijazoo mbele yetushukrani by darls babie,,, NIKI ONGOZWA NA ASURAS TECHNOLOGIES

SIMBA KUKIPIGA NA TIMU YA OLIECH JUMAMOSI

Simba SC
KATIKA kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii, mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC, Jumamosi watacheza mechi ya kujipima nguvu na Mathare United ya Kenya kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.
Habari za ndani kutoka Simba, ambazo  zimepatikana, zimesema kwamba tayari makubaliano yamefikiwa na timu timu hiyo ya Daraja la Kwanza Kenya, ambayo ilimuibua kisoka mshambuliaji wa AJ Auxerre ya Ufaransa, Dennis Oliech.
Simba itamenyana na Azam katika mechi ya Ngao ya Jamii ya kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Septemba 8, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Habari za ndani kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimesema kwamba, kuchelewa kwa mechi hiyo ambako kumeenda sambamba na kuchelewa kuanza kwa ligi hiyo, kumetokana na kuchelewa kufikiwa mwafaka mapema wa mkataba mpya wa udhamini wa Ligi Kuu.
Mkataba wa awali wa Vodacom na TFF unafikia tamati mwishoni mwa mwezi huu na kusainiwa mkataba mwingine, baada ya majadiliano yanayoendelea.
Lakini kwa kuwa Mkutano Mkuu wa TFF uliopita uliridhia kuanzia msimu ujao Ligi Kuu iendeshwe na kampuni itakayoundwa na klabu za Ligi Kuu mjadala kuhusu udhamini mpya wa ligi umekuwa mrefu kutokana na kuhusisha pande tatu, klabu, wadhamini na shirikisho.
Lakini sasa, kwa vyovyote, hata maridhiano ya mkataba mpya wa udhamini na Vodacom yachelewe tena, mechi hiyo itachezwa Septemba 8, ikiwa ni wiki moja kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.
Kihistoria hiyo itakuwa mechi ya tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili kuishirikisha timu nje ya wapinzani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba na Yanga.
Mtibwa ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na ikashinda mabao 2-1 na kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa bado inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Safari Lager, ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao kihistoria.
Katika mechi hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na mwaka juzi Yanga iliifunga tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na mwaka jana, Simba ilitwaa Ngao ya kwanza katika historia yake, kwa kuifunga Yanga mabao 2-0. 

MISS ILALA NI TAR 7 SEPTEMBER 2012




                                                      warimbwende hao wa pande za ilala
                      tarehe 30 august 2012 siku ya alhamisi , kutakuwa na mashindano ya vipaji kabla ku mpata
                      malkia ambae nata vikwa taji la mlimbwendae wa ilala

         maelezo zaidi tuta yapata kadri siku zinozo endelea kabla ya kupata malkia ambae ata vikwa taji hilo la ilala wote mna karibishwa siku hyo...!!!

HIVI NDIVYO WASHINDI WA BIBI BOMBA WALIVYOKUA WAKIJINYAKULIA ZAWADI ZAO



SHINDANO la <Bibi Bomba> lilikuwa likiratibiwa na kituo cha Clouds TV, usiku wa kuamkia leo limefikia tamati na Veronica Mpangala akiibuka mshindi wa kitita cha 5,000, 000/= (milioni tano) nafasi ya pili ilichukuliwa na Anna Saidi ambaye alijipatia kiasi cha shilingi milioni tatu, na mshindi namba tatu alikuwa ni Nasra Mohamed ambaye alijipatia kiasi cha shilingi milioni moja na nusu.

HUYU NDIYE MSHINDI WA SHINDANO LA BIBI BOMBA.......

                                                     Veronica Mpangala  a.k.a Tukinao

Vurugu zaigubika Kariakoo, mabomu yalipuliwa, Chanzo mgogoro wa nyumba,mitaa yafungwa kwa muda

HALI YA BI KIDUDE NAYO NI TETE

 
 gwiji wa muziki wa mwambao afrika fatuma binti baraka imelipotiwa kuwa hali yake kwa sasa sio nzuri kiafya mpaka kupelekewa kulazwa katika hospital ya mnazi mmoja huko zanzibar dua zetu ni kitu muhimu sana kwa bibi huyu hili hali yake irudi kawaida.amin.natumaini kila mmoja wetu ata mwombea bibi huyu ili aweze kurudi katika hali yake........by darls babie

On the cover of Baabkubwa Magazine this month...

usimchezeee diamond anapesa kama takata taka wazeiya......!!!!!!!!!

KIVUMBI COLLECTION BY MARTIN KADINDA@ DAR FASHION FESTIVAL: