Tanzania Daima ambayo ilikuwepo
katika eneo la tukio hilo ilishuhudia mamia ya vijana wakiwa wamejitokea
kwa wingi katika uzinduzi huo wa aina yake.
Aidha
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama aliwahamasisha mamia ya
mashabiki na wadau mbalimbali waliofika katika uzinduzi huouliofanyika
katika Viwanja vya Chuo Cha Ushirika kushrehekea kwa amani na utulivu
pamoja na kutosahau kujitokeza katika zoezi la sensa.
Baaadhi ya wasanii waliofunika
katika uzinduzi huo ni Shetta , Richie Mavoco, Makomando, Linah, Joh
Makini, Mwana Fa bila ya kumsaha mwanamuziki wa kimataifa ambaye pia
alikuwa mshindi wa pili katika shindano la Big Brother 2012 Prezzo
kutoka nchini kenya.
Wakati huohuo uzinduzi huo
ulinogeshwa nawasanii wa nyota wa filamu nchini ambao ni Aunt Ezekiel,
Ray Kigosi ‘Ray’, Mwenyekiti wa Bongo Movie Jacob Steven ‘JB’, Steve
Nyerere na Wema Sepetu ambao walikuwepo katika uzinduzi wakiwa ambapo
walikuwa katika msafara huo kwa minajili ya kusaka vipaji vya kucheza
filamu kwa wakaazi wa mkoani hapa.Wasanii hao ambao walitambulishwa
jukwaani
Pia waliweza kuonesha namna
wanavyoweza kunengua mbali ya kucheza filamu huku mashabiki wakimpigia
kelele Wema atingishe nyonga zake mara kadhaa nay eye alifanya hivyo na
kushangiliwa ipasavyo.
Tamasha hilo limeandaliwa na
Kampuni ya Prime Time Promotions ambayo ni Kampuni dada na Clouds Media
Group yenye maskani yake jijini Dar es Salaam.
Wasanii wengine walio onesha
uwezo wao katika uzinduzi huo ni pamoja na Juma Kassim ‘Nature’, Ferooz,
Stamina, Tash &Juru, Mr. Nice, Recho, Jambo Squard, Rich Mavocal,
Ommy Dimpoz, Godzilla na Bob Junior. Jumapili usiku Agosti 26 tamasha
hili litarindima ndani ya uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga.