Mrembo na staa wa Bongo Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo kupitia
ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram ameandika ujumbe mzuri ambao
kiukweli unaweza kukupa nguvu zaidi kufikia malengo yako kama mtu
unaejitambua.
“The more they try to slow you down on the road of purpose, the faster you have to go..!
You only meet opposition when you're going the
right way”
Kwa tafsiri isiyo rasmi anasema “kwa jinsi wanavyozidi kujaribu
kukurudisha nyuma katika njia ya mafanikio ndio inakubidi uongeze
mwendo…..na utapingigwa tu pale unapokwenda njia sahii”.
Kwa upande wangu, huu ni ujumbe mzuri sana ambao ningependa niulete hapa
kwenu wadau ili nanyinyi muuchukue kama changamoto ya kufanyikisha
mambo yako.
Asante sana Lulu kwa maneno haya mazuri.
Mzee wa Ubuyu