NYANGUMI AFNYA UHARIBIFU WA BOTI NA PIA KUJERUHI WATU
Watu watatu wamejeruhiwa baada ya Nyangumi kuibuka ghafla na kurukia boti waliyokua wakisafiria huko Eastern Cape Afrika Kusini. Boti ilikua
inakwenda polepole ghafla Nyangumi akajitokeza toka chini ya maji na
kurukia hiyo boti, waliojeruhiwa ambao baadae kidogo waliokolewa na
kikosi cha uokoaji ni mzee wa miaka 41 na abiria wengine wenye umri wa
miaka 25 na mwingine 35.