Ndege ya shirika la hifadhi la taifa (TANAPA) aina ya C182 ikiwa imeanguka katika eneo la nsemulwa mjini Mpanda muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa Mpanda ikiwa inaendeshwa na rubani Adam kajwa alieumia sehemu ya uso.
PICHA 3 ZA AJALI YA NDEGE YA TANAPA ILIYOTOKEA JANA MPANDA TANZANIA....
Ndege ya shirika la hifadhi la taifa (TANAPA) aina ya C182 ikiwa imeanguka katika eneo la nsemulwa mjini Mpanda muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa Mpanda ikiwa inaendeshwa na rubani Adam kajwa alieumia sehemu ya uso.
PICTURE OF THE DAY
nawashkuru sana wadau wangu ambao mme tembelea katika blog yangu ya darls babie na ambao mnaendelea kupata habari mbali mbali katika hii blog yangu sina cha kuwalipa zaidi ya kuwambia asanteni sana kwani bila nyie siwezi ku mimi wadau wangu naomba muendele na moyo mlo kua nao na hivi karibuni tegemeni mzigo mpya kwani kutakua na kipindi cha SWAGZ IN DAR NA RADHA ZA KITAA mtakua na mie darls babie pamoja na wengine kibao kaa mkao wa kula mna karibishwa wote asanteni sana........!!!!!!
KILICHO SABABISHA AJARI YA DIAMOND KUTOKEA
AKIONGEA BWANA NASEEB ABDUL NA DARLS BABIE NA KUNIPA USIBITISHO ZAIDI
DIAMOND
AKIONGEA......Tarehe 10 ya mwezi wa 11 siku ya juma mosi ni moja ya siku ambazo
sitozisahau maishani mwangu.
Baada
ya kumaliza majukumu yangu ya kila siku, nilikwenda masaki kumwona mmoja wa
jamaa zangu wa karibu nikiwa na Blogger wangu Bestizzo pamoja na mwanafamilkia
ya wasafi Dumi(Dancer) Mishale ya saa moja hivi nikiwa maeneo ya masaki karibu
na kona ya msasani nilipata ajali ambayo haikuwa kubwa sana ingawa imesababisha
uharibifu kwa kiasi kikubwa, Kama mjuavyo barabara ya msasani ni ndogo na gari
huwa haziko katika mwendo wa kasi... ghafla dereva wa pikipiki alikatisha mbele
yangu na katika kujaribu kumkwepa nikagonga gari ndogo aina ya Rav 4 ambapo
ilisababisha dereva wa pikipiki kuanguka katikati ya gari zote mbili. Hiyo ndio
hali halisi ya ajali niliyokutana nayo jumamosi iliyopita.
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutunusuru wote bila majeraha makubwa zaidi ya maumivu tu ya hapa na pale.
Hii ni pikipiki ambayo ni chanzo cha ajali.....
|
NYANGUMI AFNYA UHARIBIFU WA BOTI NA PIA KUJERUHI WATU
Boti ilikua inakwenda polepole ghafla Nyangumi akajitokeza toka chini ya maji na kurukia hiyo boti, waliojeruhiwa ambao baadae kidogo waliokolewa na kikosi cha uokoaji ni mzee wa miaka 41 na abiria wengine wenye umri wa miaka 25 na mwingine 35.
SHEHE SORANGA AJERUHIWA KWA KUMWAGIWA TINDIKALI.. ZANZIBAR
Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akitolewa katika Chumba
cha Huduma ya Mwanzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kurushiwa
Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika
Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akipandishwa kwenye
Gari ya Wagonjwa kwa lengo la kuwahishwa katika Hospitali ya Muhimbili
Dare es Salaam baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana
wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
DOGO ASLAY AINGIA KWENYE TUZO ZA KORA
Msanii mdogo anayekimbiza wenzake wadogo wanaokuja hapa Bongo (Aslay),
ametajwa kama msanii mpya katika tuzo za Kora mwaka huu (Best Male
Newcomer). Wimbo uliompeleka katika tuzo hizo unaitwa NIWE NAWE, Aslay
anapambana na wasanii kutoka nchi nyingine kama Uganda, Burkina Faso,
Zambia, Nigeria na Afrique Du Sud.
Mbali na Dogo Aslay tunao wasanii wengine wakubwa kutoka Tanzania hapa
kama Lady Jay Dee, Saida Karoli na Ali Kiba...
HAPPY BIRTHDAY RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR.JAKAYA MRISHO KIKWETE
Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
leo ametimiza umri wa miaka 62. Tunamtakia maisha mema rais wetu.NA marefu tena yenye manufaa
HIVI NDIVYO ILIVYO KUWA NDANI YA BIRTHDAY YA DIAMOND PLATNUM
Subscribe to:
Posts (Atom)